Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Evaclotida Kapinga (kushoto), Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa, John Wanjala (wa pili kulia) na Amos Ogunya (kulia) wakiweka shada kwenye kaburi la aliyekuwa Mtumishi wa Mamlaka, marehemu Paul Mtango wakati wa mazishi yaliyofanyika nyumbani kwao katika kijiji cha Mtii, eneo la Myombo, Same, Kilimanjaro Aprili 30, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akiaga mwili wa marehemu Paul Mtango kabla ya mazishi yaliyofanyika nyumbani kwao katika kijiji cha Mtii, eneo la Myombo, Same, Kilimanjaro Aprili 30, 2025.
Mwili wa marehemu Paul Mtango ukiwasili nyumbani kwao katika kijiji cha Mtii, eneo la Myombo, Kata ya Gonja Maore, Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro Aprili 30, 2025.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka Kanda ya Kusini, wakiwa katika uwanja wa Sabasaba Newala – Mtwara tayari kwa kushiriki maandamano ya Siku wa Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), 2025.
Watumishi wa Mamlaka kutoka kulia ni Judith Lema, Saile Kurata, Emanuel Lewanga na Benny Migire wakiwa wameshika Tuzo na Cheti cha Mshindi wa Pili baada ya kuibuka washindi wa pili kwenye kipengele cha Shughuli za Kitaaluma, za Kisayansi na Kiufundi katika Maonesho ya Kitaifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yaliyofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida kuanzia Aprili 24 hadi Aprili 30, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwapungia mkono wafanyakazi kutoka taasisi, mashirika, makampuni na wananchi waliokuwa kwenye maandamano katika Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida Mei 1, 2025.
Watumishi wa Mamlaka wakiandamana kuelekea katika viwanja vya Bombadia zilipofanyika Sherehe za Mei Mosi 2025.
Watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya ndogo ya Dar es Salaam na Ofisi ya Kanda ya Mashariki, wakiwa katika maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam, Mei 1, 2025.
Watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya ndogo ya Dar es Salaam na Ofisi ya Kanda ya Mashariki, wakiwa pamoja kwa ajili ya kuelekea kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam, Mei 1, 2025.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wakipita mbele ya jukwaa kuu katika uwanja wa CCM Sokoine kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi.