Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka, Christopher Kadio (wa tatu kutoka kulia) akiwa pamoja na Wajumbe wa Bodi alioambatana nao wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya NAK Limited, Pamela Mutabazi (katikati) akiwaelezea kuhusu namna uteketezaji wa kemikali taka unavyofanyika mara baada ya kutembelea kampuni hiyo iliyopo Fukayosi, Bagamoyo, Mkoa wa Pwani Februari 3, 2026.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Christopher Kadio (wa tano kutoka kulia) akiwa na Katibu wa Bodi, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa tatu kutoka kulia) Wajumbe wa Bodi, Meneja wa Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya NAK Limited, Pamela Mutabazi (wa tano kutoka kushoto) mara baada ya kumaliza kutembelea kampuni hiyo iliyopo Bagamoyo, Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Kadio, akikagua baadhi ya kemikali katika ghala la kuhifadhi kemikali la kampuni ya NAK limited inayojihusisha na shughuli ya uteketezaji wa kemikali taka iliyopo Fukayosi, Bagamoyo.
Katibu wa Bodi na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa tatu kutoka kulia) akimuuliza swali Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bagamoyo Sugar Limited, Sadanand Eravang (wa pili kutoka kushoto) walipotembelea maeneo ya uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho kilichopo Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, Februari 3, 2026.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka, Christopher Kadio (katikati) akiwa na Katibu wa Bodi, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa nne kutoka kulia) Wajumbe wa Bodi, Meneja wa Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Bagamoyo Sugar Limited, Sadanand Eravang (wa nne kutoka kushoto) pamoja na watumishi wa Mamlaka walioambatana nao kutembelea kiwanda cha sukari cha Bagamoyo, Februari 3, 2026.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Christopher Kadio, akizungumza na uongozi wa kampuni ya KEDS Tanzania (hawapo pichani) alipotembelea kiwanda hicho kinachotengeneza sabuni kilichopo Kibaha mkoani Pwani akiongozana na Wajumbe wa Bodi Februari 4, 2026.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka, Christopher Kadio (katikati) akiwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa tatu kutoka kulia) Wajumbe wa Bodi, watumishi wa Mamlaka pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya GRAVITA, Alok Tiwar (wa tatu kutoka kushoto) walipotembelea kampuni hiyo ya uchakataji tena wa betri na alluminium zilizotumika kilichopo Kibaha mkoani Pwani, Februari 4, 2026.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Edda Vuhahula (katikati) na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) wakiuliza maswali kuhusu usalama wa uhifadhi wa kemikali kwenye kiwanda cha KEDS Tanzania walipotembelea katika kiwanda hicho cha sabuni kilichopo Kibaha, Pwani, Februari 4, 2026.
Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Kadio (wa tano kutoka kushoto) akiwa pamoja na Wajumbe wa Bodi wakipata maelezo kuhusu utendaji kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya GRAVITA, Alok Tiwar (katikati) walipotembelea kampuni hiyo ya uchakataji (recycling) wa betri za vyombo vya moto na alluminium zilizotumika kilichopo Kibaha mkoani Pwani Februari 4, 2026.
Mjumbe wa Bodi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Saleh Ambika (kushoto) na Meneja wa Mamlaka ofisi ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa (katikati) wakipata taarifa ya utendaji kutoka kwa Afisa Utawala, David Mallya walipokuwa kwenye ziara ya ukaguzi katika kampuni ya KEDS Tanzania