Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Kitengo cha Udhibiti Ubora na Usimamizi wa Vihatarishi

Kitengo hiki kinafanya kazi zifuatazo:

  • Kutekeleza mifumo ya Usimamizi wa Ubora na matakwa ya Ithibati za Maabara;
  • Kuratibu na kufanya ukaguzi wa ndani na nje ya Usimamizi wa Mifumo ya Ubora;
  • Kuratibu na kufanya mapitio ya mara kwa mara ya usimamizi wa Mifumo ya Ubora
  • Kuratibu na kusimamia mipango ya Usimamizi wa Mifumo ya Ubora, kufanya ufuatiliaji, kutoa mafunzo na maboresho ya mara kwa mara;
  • Kufanya ufuatiliaji na mapitio ya utekelezaji wa Sheria, Viwango vya Mifumo ya Ubora vya Kitaifa na Kimataifa;
  • Kusimamia uandaaji, utekelezaji na uidhinishwaji na utunzwaji wa taratibu za uchunguzi wa kimaabara, kuratibu programu za umahiri za uchunguzi wa kimaabara na Ithibati za Maabara;
  • Kuandaa, kusimamia na kufanya tathmini ya utekelzaji wa Rejesta ya Usimamizi wa Vihatarishi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
  • Kutunza na kufanya mapitio ya utekelzaji wa Rejesta ya Usimamizi wa Vihatarishi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
  • Kutoa mafunzo kwa wataalam wa Mamlaka juu ya vihatarishi; na
  • Kutayarisha, kutumia na kuhuisha taratibu za Ukaguzi wa vihatarishi.