Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Sehemu ya Fedha na Uhasibu

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo: -

  • Kuratibu masuala yanayohusiana na usimamizi wa fedha, uhasibu na hazina;
  • Kuanzisha na kutunza vitabu vya hesabu vya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kulingana na viwango vilivyowekwa.
  • Kuratibu uandaaji wa taarifa za fedha za mwezi, robo na mwaka na ripoti kwa ajili ya ukaguzi wa ndani na nje;
  • Kuhakikisha ufanisi katika ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato na matumizi kulingana na matakwa ya bajeti na sera za fedha;
  • Kuandaa na kupitia kanuni za fedha, miongozo ya kiuhasibu na kuratibu utekelezaji wake;
  • Kuhakikisha mishahara, kodi na malipo yote ya kisheria yanatekelezwa kikamilifu.
  • Kuhakikisha shughuli za kifedha zimeingizwa katika mfumo wa usimamizi wa fedha wa pamoja (IFMS) ili kuweza kupata taarifa za fedha za mwezi, robo na mwaka ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyokamilika.
  • Kufuatilia na kudhibiti mwenendo wa mzunguko wa fedha kwenye masuala yanayohusu uwekezaji wa fedha na uwekezaji mwingine;
  • Kutayarisha, kutekeleza na kuhuisha taratibu za utendaji kazi wa sehemu ya Fedha na Uhasibu; na
  • Kushiriki katika kuandaa bajeti.