Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Sehemu ya Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia

 • Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:
 • Kufanya uchunguzi wa kitoksikolojia ili kubaini uwepo au kutokuwepo kwa sumu kwenye sampuli/vielelezo vya vyakula, baiolojia (mfano mkojo, matumbo, damu, matapishi, figo, utumbo mpana na wengu), maji, udongo, mimea na sampuli nyinginezo zinazohusiana na makosa ya jinai;
 • Kubaini kiwango cha sumu kwenye sampuli/vielelezo vya vyakula, baiolojia (mfano mkojo, matumbo, damu, matapishi, figo, utumbo mpana na wengu), maji, udongo, mimea na sampuli nyinginezo zinazohusiana na makosa ya jinai;
 • Kufanya uchunguzi wa kilevi kwenye sampuli za kibailojia ili kubaini endapo mtu alitumia kilevi kabla ya tukio na iwapo kiwango cha kilevi hicho kimeweza kuathiri tabia ya muhusika;
 • Kufanya utafiti na kutoa ushauri katika masuala yanayohusiana na kazi za Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia;
 • Kutoa ushahidi wa kitaalam kwenye Mahakama unaohusiana na uchunguzi wa Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia;
 • Kutoa elimu kwa wataalam juu ya taratibu za uchukuaji na usimamizi wa sampuli za toksikolojia;
 • Kufanya uchunguzi wa kitoksikolojia unaohusiana na masuala yenye maslahi ya jamii na Taifa;
 • Kuandaa, kutathmini na kufanya mapitio ya mbinu za uchunguzi wa Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia
 • Kutayarisha, kutumia na kufanya mapitio ya taratibu za uchunguzi wa Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia
 • Kushiriki kwenye uchunguzi wa kujipima umahiri ili kuwajengea uwezo na ujuzi wataalamu wa Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia;