Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Sehemu ya Maabara ya Maikrobaiolojia

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo: -

  • Kufanya uchunguzi wa kimaikrobaiolojia wa vyakula, maji, dawa na malighafi zake, sabuni, kemikali za kutibu maji, dawa asili, viungo na bidhaa nyingine zilizosindikwa na zisizosindikwa;
  • Kuandaa, kuhakiki mbinu za uchunguzi na mapitio ya njia za uchukuaji wa sampuli na uchunguzi wa kimaikrobaiolojia wa vyakula, dawa na malighafi zake, dawa asili, sabuni, kemikali za kutibu maji, viungo na bidhaa nyingine zilizosindikwa na zisizosindikwa;
  • Kutayarisha, kutumia na kufanya mapitio ya taratibu za uchunguzi wa kimaabara katika Maabara ya Maikrobaiolojia;
  • Kufanya utafiti katika masuala yanayohusiana na Maabara ya Mikrobaiolojia
  • Kutayarisha, kutumia na kufanya mapitio ya miongozo ya uchunguzi wa Maabara ya Maikrobaiolojia;
  • Kushiriki kwenye uchunguzi wa kujipima umahiri ili kuwajengea uwezo na ujuzi wataalamu wa Maabara ya Maikrobaiolojia;
  • Kutoa ushauri wa kitaalam katika masuala yanayohusiana na kazi za Maabara ya Maikrobaiolojia; na
  • Kufanya ukaguzi wa dharura, uchukuaji na uchunguzi wa maikrobaiolojia wa sampuli za vyakula, dawa na malighafi zake, dawa asili, viungo na bidhaa nyingine zilizosindikwa na zisizosindikwa zinazohusiana na maslahi ya jamii au Taifa.