Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Kitengo cha Ukaguzi wa ndani

Kitengo hiki kinafanya kazi zifuatazo: -

  • Kupitia sera, mipango, taratibu, sheria na kanuni ambazo zinaweza kuleta matokeo chanya katika uendeshaji wa Mamlaka ili kubaini iwapo Mamlaka inatekeleza Sheria, Kanuni na Taratibu na maelekezo yanayotolewa;
  • Kupitia mifumo iliyoanzishwa ndani ya Mamlaka ili kuhakikisha kama inafuata sera, mipango, taratibu, sheria na kanuni ambazo zinaweza kuleta matokeo chanya katika uendeshaji wa Mamlaka ili kubaini iwapo Mamlaka inatekeleza Sheria, Kanuni na Taratibu na maelekezo yanayotolewa.
  • Kupitia na kufuatilia mfumo wa usimamizi wa vihatarishi ili kuhakikisha kuwa vihatarishi vinatambuliwa na kusimamiwa ipasavyo;
  • Kupitia michakato ya utawala ili kuhakikisha kuwa mwingiliano na vikundi anuwai vya utawala unakuwepo kama unavyohitajika;
  • Kupitia upatikanaji na uadilifu wa taarifa za kifedha na njia zinazotumiwa kutambua, kupima, kuainisha na kuripoti za taarifa hizo;
  • Kupitia njia za kulinda mali za Mamlaka kama inavyohitajika, na kuthibitisha uwepo wa mali hizo;
  • Kupitia na kutathmini uchumi, ufanisi na uimara wa rasilimali zinazotumika ndani ya Mamlaka; na
  • Kupitia uendeshaji na programu za Mamlaka ili kubaini ikiwa matokeo yanaendana na malengo na ikiwa uendeshaji au  programu zinatekelezwa  kama