Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Sehemu ya Maabara ya Mazingira

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo: -

  • Kufanya uchunguzi wa kikemia wa maji na maji taka, udongo, miamba, mboga mboga, samaki, kemikali taka, damu, mkojo, sabuni, vipodozi, kemikali na bidhaa zake.
  • Kuandaa, kuhakiki mbinu za uchunguzi na mapitio ya njia za uchukuaji wa sampuli na uchunguzi wa kikemia wa maji na maji taka, udongo, miamba, mboga mboga, samaki, kemikali taka, damu, mkojo, sabuni, vipodozi, kemikali na bidhaa zake.
  • Kutayarisha, kutumia na kufanya mapitio ya taratibu za uchunguzi wa kimaabara wa kemikali na bidhaa zake.
  • Kufanya utafiti katika masuala yanayohusiana na kemikali na bidhaa zake, usalama wa mazingira na usalama wa afya mahali pa kazi.
  • Kutayarisha miongozo na taratibu za usimamizi na uteketezaji wa kemikali zilizoisha muda wake.
  • Kushiriki kwenye uchunguzi wa kujipima umahiri ili kuwajengea uwezo na ujuzi wataalamu wa maabara.
  • Kutoa ushauri wa kitaalam katika masuala yanayohusiana na kazi za maabara ya mazingira.
  • Kufanya ukaguzi wa dharura, uchukuaji na uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za mazingira, usalama mahali pa kazi, kemikali na bidhaa zake zinazohusiana na maslahi ya jamii au Taifa.