Sehemu ya Maabara ya Chakula na Dawa
Sehemu ya Maabara ya Chakula na Dawa
Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo: -
- Kufanya uchunguzi wa kikemia wa vyakula, dawa na malighafi zake, dawa asili, viungo na bidhaa nyingine zilizosindikwa na zisizosindikwa;
- Kuandaa, kuhakiki mbinu za uchunguzi na mapitio ya njia za uchukuaji wa sampuli na uchunguzi wa kikemia wa vyakula, dawa na malighafi zake, dawa asili, viungo na bidhaa nyingine zilizosindikwa na zisizosindikwa;
- Kutayarisha, kutumia na kufanya mapitio ya taratibu za uchunguzi wa kimaabara wa kemikali na bidhaa zake;
- Kufanya utafiti katika masuala yanayohusiana na maabara ya chakula na dawa;
- Kutayarisha, kutumia na kufanya mapitio ya miongozo ya uchunguzi wa maabara ya Chakula na Dawa;
- Kushiriki kwenye uchunguzi wa kujipima umahiri ili kuwajengea uwezo na ujuzi wataalamu wa maabara ya Chakula na Dawa;
- Kutoa ushauri wa kitaalam katika masuala yanayohusiana na kazi za maabara ya Chakula na Dawa; na
- Kufanya ukaguzi wa dharura, uchukuaji na uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za vyakula, dawa na malighafi zake, dawa asili, viungo na bidhaa nyingine zilizosindikwa na zisizosindikwa zinazohusiana na maslahi ya jamii au Taifa