Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Kituo cha uthibiti wa sumu kitaifa

Kitengo cha Taifa cha Kudhibiti Sumu (NPCC)-kilianzishwa na Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Kemia ya Serikali Namba 8 ya 2016, kusimamia na kuratibu visa vyote  vya sumu kwa kutoa huduma za habari za sumu; kwa lengo la kupunguza vifo na magonjwa kutokana na sumu nchini. Bonyeza hapa KUPAKUA>>>NPCC VIPEPERUSHI

Kituo kinafanya kazi zifuatazo;

  • Kuwasiliana na kukusanya taarifa za kimaabara za sumu kutoka maabara za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Hospitali za Rufaa, mikoa, pamoja na vituo vya Polisi, kusimamia utoaji wa taarifa na ushauri kuhusu utambuzi, tiba na kuzuia sumu zikiwemo sumu za kemikali na athari zake;
  • Kuandaa na kuisimamia Kanzidata ya Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Sumu (NPCC);
  • Kuratibu shughuli za tahadhari za sumu;
  • Kufanya tafiti, kutoa elimu na mafunzo kwa wadau kuhusu kuzuia matukio ya sumu;
  • Kuandaa mpango wa dharura, kufuatilia na kujibu athari mbaya za dawa ikiwemo matatizo ya matumizi yasiyo sahihi ya dawa;
  • Utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa bora; na
  • Kuandaa, kutekeleza na kuhuisha miongozo na Taratibu za Utendaji Kazi ya Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Sumu.

CONTACT:  To report incidents of poisoning: Toll Free 0800112031