Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma

Kitengo kinafanya kazi zifuatazo:

 • Kuandaa na kutekeleza Mpango wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma;
 • Kusimamia uratibu wa programu za vyombo vya habari;
 • Kuratibu maandalizi ya Taarifa kwa Vyombo vya Habari, Hotuba na Makala;
 • Kuhamasisha na kutangaza huduma za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa Umma;
 • Usimamizi na uhuishaji wa Tovuti ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
 • Kuratibu ushiriki wa matukio na maonesho mbalimbali;
 • Kuratibu maandalizi ya utengenezaji wa Kalenda, Makala, Vipeperushi, Taarifa kwa mteja na Jarida la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
 • Kuratibu usimamizi wa malalamiko ya mteja kwenye Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali;
 • Kuandaa, kutekeleza na kuhuisha taratibu za utendaji kazi za Uhusiano kwa Umma;
 • Kuratibu mafunzo au uhamasishaji wa huduma kwa mteja;
 • Ufuatiliaji wa shughuli za matangazo na kujitangaza; na
 • Kupitia, kushauri na kutelekeza mpango wa masoko na mikakati ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.