Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akizungumza wakati akifungua Kikao cha nne cha Baraza la nane la Wafanyakazi ambapo walikutana kujadili utekelezaji wa Mipango ya Mamlaka kwa Mwaka wa Fedha wa 2025/2026 kilichofanyika Cate Hoteli mkoani Morogoro Oktoba 9, 2026. Kushoto ni Katibu wa Baraza, Florida Tumbu na kulia ni Katibu Msaidizi wa Baraza, Rotani Kibaza.
Mjumbe wa Baraza, Nancy Nombo, akitoa wasilisho la sera ya Utoaji wa Taarifa kwa Siri (Whistleblower policy), katika kikao cha Nne cha Baraza la Nane la Wafanyakazi wa Mamlaka kilichofanyika Cate Hoteli mkoani Morogoro Oktoba 9, 2026.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Fedha, Abely Mushi, akiwaslisha mada kuhusu Uendelevu wa Mazingira, Jamii na Utawala (Environmental, Social, Governance Sustainability) kwa wajumbe wa kikao cha Baraza katika kikao cha nne cha Baraza la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kilichofanyika Cate Hoteli mkoani Morogoro Oktoba 9, 2026.
Mwenyekiti wa Baraza, Dkt. Fidelice Mafumiko (katiikati) akifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na wadau kutoka Wizara ya Fedha (Hawapo Pichani), iliyohusu uendelevu wa Mazingira, Jamii na Utawala (Enviromental, Social,Governance Sustainability) katika kikao cha nne cha Baraza la Nane la Wafanyakazi kilichofanyika Cate Hoteli mkoani Morogoro Oktoba 9, 2026.
Mwenyekiti wa Kamati wa Tendaji ya Baraza, Benny Mallya, akiwasilisha mada kuhusu waliyoyaona kwenye Kamati kuhusiana na utekelezaji wa Mpango wa Mamlaka wa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na kutoa maoni ya namna ya kufanya maboresho kwa miaka mingine katika Kikao cha nne cha Baraza la nane la Wafanyakazi kilichofanyika Cate Hoteli mkoani Morogoro Oktoba 9, 2026.
Mjumbe wa Baraza ambaye ni Mwakilishi kutoka TUGHE Taifa, Shadrack Mkodo, akitoa taarifa kutoka TUGHE Taifa na kulipongeza Baraza la Mamlaka kwa kutimiza majukumu yao ipasavyo katika Kikao cha nne cha Baraza la nane la Wafanyakazi kilichofanyika Cate Hoteli mkoani Morogoro Oktoba 9, 2026.
Wajumbe wa Baraza wakiufatilia Kikao cha nne cha Baraza la nane la Wafanyakazi kilichofanyika Cate Hoteli mkoani Morogoro Oktoba 9, 2026.
Mwenyekiti wa Baraza, Dkt. Fidelice Mafumiko, (Katikati), Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti Daniel Ndiyo (wa Nne Kushoto), Katibu wa Baraza Florida Tumbu (wa nne kulia), Katibu Msaidizi wa Baraza Rotani Kibaza (wa Pili Kulia) wakiwa wameshika tuzo tatu ambazo Mamlaka ilishinda katika Maonesho ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika mkoani Geita na kukamilika Oktoba 3, 2026. Tuzo hizo zimekabidhiwa katika kikao cha Baraza kilichofanyika Cate Hoteli mkoani Morogoro Oktoba 9, 2026.
Mwenyekiti wa Baraza, Dkt.Fidelice Mafumiko (Katikati) akiwa pamoja na Wajumbe wa kikao cha nne cha Baraza la Nane la Wafanyakazi mara baada ya kukamilika kwa kikao hicho ambapo walikutana kujadiliana utekelezaji wa Mipango ya Taasisi kwa Mwaka wa Fedha wa 2025/2026 kilichofanyika Cate Hoteli mkoani Morogoro Oktoba 9, 2026.
Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa, akizungumza na wateja pamoja na watumishi wa Mamlaka wakati akifungua hafla fupi ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa mteja,iliyofanyika katika Ofisi ya Kanda ya Mashariki, jijini Dar es Salaam, Oktoba 8, 2026.