Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Sehemu ya Ukaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia

Sehemu hii inafanya kazi zifuatazo:

 • Kutayarisha mipango ya ukaguzi, miongozo na dodoso kwa ajili ya ukaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia;
 • Kuratibu na kufanya ukaguzi kwa wazalishaji, waingizaji, wasafirishaji ndani na nje ya nchi na wadau wengine wanaojihusisha na kemikali;
 • Kuratibu na kufanya ukaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia;
 • Kuratibu, kusimamia na kudhibiti uingizaji, uzalishaji, usafirishaji, utumiaji, utunzaji na utekelezaji;
 • Kuratibu ukaguzi wa kemikali na Maabara za Kemikali kwenye Ofisi za Kanda;
 • Kuratibu Mikutano ya Kamati ya Dharura ya Kemikali;
 • Kuratibu utekelezaji wa Mikataba ya Kimataifa ya Basel, Rotterdam na Stockholm (BRS) inayohusiana na kemikali;
 • Kufanya kampeni ya kuhamasisha umma juu ya usimamizi wa kemikali;
 • Kutoa mafunzo maalum kwa wakaguzi wa kemikali na Maabara za Kemia ili waweze kutangazwa kwenye gazeti la Serikali;
 • Kupendekeza Kanuni mpya na kufanya mapitio ya Kanuni zinazohusiana na kemikali na maabara za kemia; na
 • Kufuatilia utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali Na.3 ya Mwaka 2003, Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Na.8 ya Mwaka 2016 na Kanuni zake.