Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika makazi ya watumishi katika mpaka wa Holili uliopo Wilaya ya Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kanda ya Kaskazini, Machi 3, 2026.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia) akisalimiana na Mkaguzi wa Kemikali wa Mamlaka katika Mpaka wa Holili, Jackson Chaula (kushoto) mara baada ya kufika katika makazi ya watumishi katika mpaka huo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kanda ya Kaskazini, Machi 3, 2026.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa kofia) akiwa pamoja na Kaimu Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Joshua Mustafa, wakati akikagua nyumba ya watumishi katika Mpaka wa Holili wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kanda ya Kaskazini, Machi 3, 2026.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia) akiongea na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mark Beverages Ltd, Kelvin Laswai (kushoto) mara baada ya kufika kwa ajili ya ukaguzi kwenye kampuni hiyo inayotengeneza pombe kali iliyopo Moshi, mkoani Kilimanjaro, Machi 3, 2026.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa kofia) akikagua maabara ya kampuni ya Mark beverages Ltd inayotengeneza pombe iliyopo Moshi, mkoani Kilimanjaro, Machi 3, 2026.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa kofia) na Kaimu Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Joshua Mustafa (aliyevaa miwani), wakikagua maeneo ya utengenezaji wa pombe katika kampuni ya Mark Beverages Ltd wakati wa ukaguzi uliofanyika Machi 3, 2026, Moshi mkoani Kilimanjaro.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Toba Nguvila (kushoto) akiongea na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia) mara baada ya kufika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kumsalimia, Machi 4, 2026.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akiongea na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Eliamini Mkenga (kulia) mara baada ya kufika katika Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Machi 4, 2026.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akimsikiliza Mjasiriamali Bartholomeo Shawuri (kulia) akimueleza namna anavyotengeneza pombe kali kwa kutumia kemikali aina ya ethanol mara baada ya kumtembelea katika eneo lake la biashara jijini Arusha Machi 4, 2026.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia), akiongea na Mkurugenzi wa kiwanda cha A to Z Group Ltd, Binesh Haria (kushoto) mara baada ya kufika katika kiwanda hicho kilichopo jijini Arusha Machi 4, 2026.