Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

TARATIBU ZA KUPATA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA VINASABA

01 Jun, 2023

Taratibu za kupata huduma za uchunguzi wa vinasaba

Huduma za uchunguzi wa vinasaba hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009.Taratibu zifuatazo hufuatwa ili kuweza kupata huduma za uchunguzi;-

1. Mteja anayehitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa Vinasaba anawakilishwa na taasisi zilizotajwa kwenye sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya Mwaka 2009 ili kumuombea mteja husika huduma za uchunguzi

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) cha Sheria ya vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009, taasisi zinazoruhusiwa kumuombea mteja kupatiwa huduma za uchunguzi wa vinasabani pamoja na

  • Maafisa ustawi wa jamii,
  • Mawakili,
  • Mahakama katika uchunguzi unaolenga kutataua migogoro,
  • Jeshi la polisi kwa masuala yanayohusu jinai,
  • Madakatari kwa uchunguzi unaihusiana na tiba,
  • Wakuu wa Wilaya
  • Taasisi za Tafiti zinazotambuliwa Kisheria

3. Taasisi hizo zitaandika barua za maombi ya kupatiwa huduma za uchunguzi kwa niaba ya mteja husika. Barua zote zitaandika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali.

4. Malipo ya uchunguzi ni Tsh100, 000/=kwa sampuli ya mtu mmoja, hivyo kwa uchunguzi wa Baba,Mama na Mtoto jumla niTsh.300,000/=. Malipo yote hufanyika Benki .

5. Baadaya ya kukamilisha taratibu za malipo, sampuli za mpanguso wa kinywa(Buccal swab ) zitachukuliwa na watalaam katika maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi kulingana na Maombi ya Mteja

6. Uchunguzi utafanyika na utakapokamilika majibu ya uchunguzi yatatolewa kwa taasisi iliyoandika barua ya maombi ya kufanyiwa uchunguzi na mteja husika atapata majibu yake kupitia taasisi hizo zilizoruhusiwa kisheria.

7. Majibu ya uchunguzi hutolewa kuanzia siku ya kumi na nne za kazibaada ya kuchukuliwa kwa sampuli.