Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

SIKU YA VINASABA YATIKISA, WADAU WAJADILI VIFAA TIBA

Imewekwa: 29 Apr, 2026
SIKU YA VINASABA YATIKISA, WADAU WAJADILI VIFAA TIBA

 Wadau wa sekta ya afya, utafiti na sayansi ya Vinasaba wameitumia siku ya Vinasaba kujadili umuhimu wa uuzaji na usambazaji sahihi wa vifaa tiba na vitendanishi huku wakisema kuwa ni msingi muhimu katika kuimarisha huduma za afya na maendeleo ya tafiti za kisasa Nchini.

Akizungumza Katika Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali (GCLA) yaliyofanyika tarehe 23 na 24 Aprili, 2026, katika Ukumbi wa Jakaya kiwete Jijini Dodoma, Joseph Masanja, kutoka taasisi ya usambazaji wa vifaa tiba ya Encore Medics alisema kuwa ubora wa vifaa tiba ni nguzo muhimu  katika mafanikio ya tafiti na huduma za afya kwani itaweza kuwajengea hali ya kujiamini wafanyaji utafiti wakati wakiwa katika maabara zao.

“Uuzaji na usambazaji  wa vifaa tiba vyenye viwango ni muhimu katika kuimarisha uchunguzi ,tiba na maendeleo ya sayansi ya vinasaba na pindi teknolojia ya vifaa vya uchunguzi wa vinasaba unavozidi kukuwa utaongeza hali ya kujiamini na kuongeza ufanisi mkubwa katika kazi zao” alisema Masanja.

Mdau kutoka taasisi inayohusika na Uuzaji na usambazji wa vifaa tiba Nchini (Pyramid Pharma limited), Eliud Burchad, anaamini kuwa mawazo yake ambayo amewasilisha katika siku hiyo ya maadhimisho ya siku ya vinasaba  yataleta mabadiliko chanya katika upande wa vifaa vinavyotumika kufanyia uchunguzi  wa Vinasaba vya Binadamu na mimea  huku akiamini kuwa teknolojia hiyo italeta ubora wa  ushindani  wa matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kufanya uchunguzi.

“Uuzaji na usambazaji  wa vifaaa tiba vyenye viwango ni muhimu katika kuimarisha uchunguzi wa kisayansi, nikiwa miongoni mwa wataalamu kutoka katika ofisi ya usambazaji wa vifaa vya kufanyia uchunguzi tumefanya tafiti nyingi ili kuona ni namna gani tunaweza kuwa na teknolojia ya kisasa katika kuboresha uhifadhi na namna ya uchukuaji wa sampuli mbalimbali, tukapata wazo la matumizi ya teknolojia ya kisasa ambayo inatumiwa na baadhi ya nchi mfano Afrika Kusini ambayo itatusaidia sana katika kuboresha uhifadhi wa Vinasaba,” alisema Sagalawa.

Naye Mdau kutoka taasisi binafsi ya uchunguzi wa afya na vinasaba (SERENOX AFRICA) Eliud Buchard,amesema kuwa matumizi ya teknolojia za kisasa katika uchunguzi wa Maabara na Vinasaba yanaendelea kuboresha sekta ya afya ,huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za utafiti ,sekta binafsi na vijana katika kukuza ubunifu wa kisayansi.