Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

MKEMIA MKUU WA SERIKALI ATEMBELEA SABASABA

Imewekwa: 10 Jul, 2026
MKEMIA MKUU WA SERIKALI ATEMBELEA SABASABA

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt Fidelice Mafumiko ametembelea maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam “SabaSaba” na kujionea Huduma mbalimbali zinazotolewa katika mabanda ya Wizara,Taasisi za Umma, Taasisi Binafsi na Wajasiliamali mbalimbali wanaoshiriki maonesho hayo yanayofanyika katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere.

Akizungumza baada ya kutembelea Banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili Julai 6 2026, Mkemia Mkuu wa Serikali ameameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa huduma bora za kibingwa na ubingwa bobezi inazoendelea kutoa kwa wananchi katika maonesho hayo huku akiwataka wananchi kujitokeza kupata huduma.

Baada ya Kutembelea Banda ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Mafumiko amesema Mamlaka inaendelea kushirikiana na Chuo hicho katika Nyanja ya utafiti wa Kisayansi na utoaji wa Elimu ya Matumizi sahihi na salama ya Kemikali

“Tunashirikiana kwenye eneo la Tafiti na ugunduzi ili kuchochea maendeleo katika Taifa letu, tunafahamu hapa wanazalishwa wataalamu wengi wa Sayansi hivyo kuna matumizi ya Kemikali kwa hiyo tunashirikiana pia kwenye Elimu hii ya matumizi sahihi na salama ya Kemikali” alisema Dkt. Mafumiko.

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali ametembelea banda la Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)ambapo ameipongeza Mamlaka hiyo kwa kufanyakazi kubwa ya kizalendo

“Nawapongeza sana kwa kazi nzuri ya kutoa elimu lakini kubwa zaidi kazi ya kujitolea ya kizalendo mnaoifanya chini ya Kamishna Jenerali, Aretas Lyimo ambaye tunashirikiana kwa ukaribu mkubwa” alisema Dkt. Mafumiko

Aidha Dkt. Mafumiko amewapongeza Watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuendelea kutoa huduma na Elimu kwa Wananchi katika maonesho hayo ya SabaSaba.

Kwa upande wa Daktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt Garvin Kweka na Asha Athumani kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Saalam wamemshukuru Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutembelea katika maonesho hayo.