Wajumbe wa Kamati ya Kitaalam ya Vinasaba vya Binadamu wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu (aliyesimama) akiongea wakati akizindua Kamati hiyo jijini Dodoma.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Kitaalam ya Vinasaba vya Binadamu, akitoa salamu za utangulizi kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu (hayupo pichani) kuzindua Kamati hiyo, Mei 6, 2024 jijini Dodoma.
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaalam ya Vinasaba vya Binadamu, akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu (hayupo pichani) baada ya kuzindua Kamati hiyo, Mei 6, 2024 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu (aliyesimama) akiongea wakati akizindua Kamati ya Kitaalam ya Vinasaba vya Binadamu (Human DNA Technical Committee) katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dodoma, Mei 6, 2024.
Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora na Usimamizi wa Vihatarishi, Benny Mallya kutoka GCLA (katikati), akiwa pamoja na washiriki wengine wa michezo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) baada ya kumaliza matembezi.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakiongozwa na Meneja Rasilimali Watu na Utawala, Nancy Nombo (wa pili kulia), wakiwa katika mazoezi kuelekea Coco Beach.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wanamichezo (hawapo pichani), walioshiriki matembezi na mazoezi ya kilomita 10 yaliyoanzia Coco Beach hadi mzunguko wa Hospitali ya Agha Khan na kurudi Coco Beach kwa lengo la kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza Mei 4, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kutoka kushoto), akiwa pamoja na Mbunge wa Kawe, Mhe. Josephat Gwajima (wa pili kulia), Mwamuzi wa mpira wa miguu wa zamani, Othman Kazi (kulia) wakifanya mazoezi mepesi baada ya kumaliza matembezi ya kilomita 10,kwa lengo la kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika Mei 4, 2024.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (katikati), akiongoza viongozi na wanamichezo katika mazoezi na matembezi ya kilomita 10, kwa lengo la kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yaliyofanyika Mei 4, 2024.
Watumishi wa Mamlaka Ofisi ndogo ya Dar Es Salaam na Kanda ya Mashariki wakiwa kwenye maandamano ya Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambapo kwa Mkoa wa Dar Es Salaam yalifanyika katika uwanja wa Uhuru,Mei 1,2024.