Wanamichezo wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, wakiwa pamoja na kombe na medali walizopata kwenye mashindano ya Shimmuta 2023 jijini Dodoma.
Mhe. Rosemary Senyamule akimkabidhi kombe la mshindi wa pili kwenye mbio za magunia Sholastika Hyera (kushoto), kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA).
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (kulia), akimvisha medali ya mshindi wa tatu kwenye mbio za mita 5000, Upendo Mwakifumbwa kutoka GCLA.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (wa pili kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Michezo GCLA, Sabas Mandari (kushoto) cheti cha ushiriki wa Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kwa mwaka 2023, Dodoma.
Viongozi kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakiwa pamoja na baadhi ya Maafisa wa Polisi na Waendesha Mashtaka baada ya kukamilisha mafunzo ya usimamizi wa sampuli za jinai yaliyofanyika Novemba 4, 2023, jijini Mwanza.
Kaimu Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia, Kagera Ng’weshemi (kulia) akitoa elimu juu ya uchukuaji, uhifadhi na usafirishaji salama wa vielelezo kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara.
Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mwanza, Henry Sebastian Mbilinyi (aliyesimama), akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Usimamizi wa Sampuli za Jinai yaliyotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kufanyika katika ukumbi wa Polisi – Mwanza, Novemba 4, 2023. Zaidi ya maafisa Polisi na Waendesha Mashtaka 30 walishiriki mafunzo hayo.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) wakipongezana na watumishi wa Mamlaka baada ya kupokea tuzo ya ushindi wa kwanza kwenye kipengele cha Taasisi Wezeshi za Serikali katika Sekta ya Madini kwenye Maonesho ya Madini yaliyofanyika mkoani Geita. Tuzo hiyo imekabidhiwa Oktoba 18, 2023, Dodoma.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (mbele, kushoto) akipokea tuzo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, Sabanitho Mtega (kulia) baada ya Mamlaka kuibuka washindi wa kwanza kwenye kipengele cha Taasisi Wezeshi za Serikali katika Sekta ya Madini kwenye Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika Septemba 18 – 30, 2023 mkoani Geita. Tuzo hiyo imekabidhiwa Oktoba 18, 2023, Makao Makuu ya Mamlaka, Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, cheti cha udhamini wa Kongamano la Pili la Wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linalofanyika kuanzia Septemba 12 - 15, 2023, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) uliopo jijini Arusha. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama.