Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Kanuni Ndogondogo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mihayo Nhunga, akizungumza wakati wa ziara waliyofanya ya kutembelea Maabara za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Darc es Salaam Oktoba 22, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Farid Mpatani (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa kamati na viongozi wa Mamlaka wakati wa ziara ya Kamati ya Sheria na Kanuni ndogondogo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyofanyika Oktoba 22, 2024 katika ofisi za Mamlaka, jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias, akielezea majukumu ya Mamlaka kwa Kamati ya Sheria na Kanuni Ndogo ndogo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kutembelea maabara za Mamlaka iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2024.
Wajumbe wa Kamati ya Sheria na Kanuni Ndogo ndogo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakielezwa na Wataalam wa Mamlaka namna maabara za Sayansi Jinai Kemia, Toksikolojia na Mitambo mbalimbali inavyofanya kazi kwenye maabara hizo wakati wa ziara ya kutembelea Mamlaka, Ofisi ndogo ya Dar es Salaam iliyofanyika Oktoba 22, 2024.
Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo, akizungumza na wadau mbalimbali wa uzalishaji bidhaa za rangi katika Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Kudhibiti Sumu ya Madini ya Risasi. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam Oktoba 25, 2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaalam ya Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu, Profesa Amos Mwakigonja, akizungumza na wadau katika kikao kilichofanyika siku ya Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Kudhibiti Sumu ya Madini ya Risasi Oktoba 25, 2024, jijini Dar es Salaam.
Wadau walioshiriki kikao cha Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Kudhibiti Sumu ya Madini ya Risasi, wakiuliza maswali pamoja na kutoa shukrani kwa viongozi wa Mamlaka kwa kuandaa kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam Oktoba 25, 2024.
Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu, Yohana Goshashy (aliyesimama) akizungumza wakati wa utambulisho na ukaribisho wa wadau katika Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Kudhibiti Sumu ya Madini ya Risasi.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Geita, Lusajo Mwasalyanda,(kulia) akizungumza wakati akifungua mafunzo ya namna bora ya uchukuaji, uhifadhi na usafirishaji wa sampuli zinazohusiana na jinai, uchunguzi wa sumu kwa Maafisa Upelelezi Mkoa wa Geita yaliyofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Polisi Geita Oktoba 24,2024
Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia, Kagera Ng’weshemi (aliyesimama), akiwasilisha mada katika mafunzo ya namna bora ya uchukuaji, uhifadhi na usafirishaji wa sampuli zinazohusiana na jinai na uchunguzi wa sumu kwa Maafisa Upelelezi Mkoa wa Geita yaliyofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Polisi Geita, Oktoba 24,2024.