Wadau wa kemikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo ya usimamizi salama wa kemikali kwa wadau wa kemikali yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Mafumiko jijini Dodoma Novemba 28,2024.
Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Gerard Meliyo (aliyesimama), akiwasilisha mada kuhusu Sheria na Kanuni za Usimamizi wa Kemikali za Viwandani na Majumbani katika mafunzo ya usimamizi salama wa kemikali kwa wadau wa kemikali yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Mafumiko jijini Dodoma Novemba 28,2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Musa Kuzumila (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika mafunzo ya usimamizi salama wa kemikali kwa wadau wa kemikali yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Mafumiko jijini Dodoma Novemba 28,2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Musa Kuzumila, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa Wadau wa kemikali yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Mafumiko jijini Dodoma Novemba 28,2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Musa Kuzumila (aliyekaa katikati), akiwa pamoja na wadau wa kemikali walioshiriki mafunzo ya matumizi salama ya kemikali pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Meneja wa Mamlaka Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa (aliyekaa katikati) akiwa pamoja na washiriki wa mafunzo kuhusu majukumu ya Mamlaka kwa kundi la Mawakala wa Forodha katika Kanda ya Mashariki.
Mawakala wa Forodha wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa na wataalam kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Kemia, Fidelis Segumba (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu Usimamizi wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu kwa Mawakala wa Forodha katika mafunzo kuhusu majukumu ya Mamlaka yaliyofanyika Dar es Salaam Novemba 28, 2024.
Meneja wa Mamlaka Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa (kulia), akizungumza wakati akifungua mafunzo kuhusu majukumu ya Mamlaka kwa Mawakala wa Forodha yaliyofanyika katika ukumbi wa Zimamoto, Bandari jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2024.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi, akizungumza katika kikao cha kuhitimisha Kampeni ya utoaji elimu kwa Umma juu ya Usafirishaji salama wa kemikali ya Sodium Cyanide kilichofanyika katika ukumbi wa Dkt. Mafumiko jijini Dodoma Novemba 23,2024.