Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kushoto) alipotembelea banda la Mamlaka kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya yaliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma Juni 26, 2025.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lymo (kushoto) akimkabidhi Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia), cheti cha ushiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya yaliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma Juni 26, 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (kulia), akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) alipotembelea banda la Mamlaka kwenye kilele cha Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya yaliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma Juni 26, 2025.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimia viongozi alipowasili katika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya yaliyofanyika Juni 26, 2025.
Afisa mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ally Kitumbu, (aliyesimama), akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Uchukuaji, Ukusanyaji, Utunzaji na Usafirishaji wa Sampuli za Jinai kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Wapelelezi Mkoa wa Njombe, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Polisi Jamii mkoani humo, Juni 20, 2025.
Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Kemia, Joyce Njisya, akiwasilisha mada kuhusu Uchukuaji, Uwasilishaji, na Uhifadhi wa Sampuli zinazohusiana na dawa za kulevya kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Wapelelezi wa Mkoa wa Njombe (hawapo pichani), wakati wa mafunzo ya Uchukuaji, Ukusanyaji, Utunzaji na Usafirishaji wa Sampuli za jinai kwa Maafisa hao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Polisi Jamii mkoani wa Njombe, Juni 20, 2025.
Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Baiolojia na Vinasaba, Dkt. Fidelis Bugoye, akiwasilisha mada kuhusu Uchukuaji na Ufungishaji wa Sampuli za Jinai, pamoja na namna ya kutafsiri matokeo ya Uchunguzi kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Wapelelezi (hawapo pichani), katika mafunzo Uchukuaji, Ukusanyaji, Utunzaji na Usafirishaji wa Sampuli za jinai kwa Maafisa hao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Polisi Jamii mkoani Njombe, Juni 20, 2025.
Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia, Kagera Ng’weshemi, akiwasilisha mada kuhusu Uchukuaji, Uwasilishaji, na Uhifadhi wa Sampuli zinazohusiana na sumu kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Wapelelezi wa Mkoa wa Njombe (hawapo pichani), katika mafunzo ya Uchukuaji, Ukusanyaji, Utunzaji na Usafirishaji wa Sampuli za jinai kwa Maafisa hao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Polisi Jamii mkoani wa Njombe, Juni 20, 2025.
Maafisa wa Jeshi la Polisi na Wapelelezi Mkoa wa Njombe, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo ya Uchukuaji, Ukusanyaji, Utunzaji na Usafirishaji wa Sampuli za jinai kwa Maafisa hao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Polisi Jamii mkoani Njombe, Juni 20, 2025.
Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea (kulia) akikabidhi cheti cha pongezi kwa mmoja ya wanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo ya sayansi wakati wa hafla ya kuwapongeza Wanafunzi na Walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati waliohitimu kidato cha nne mwaka 2023 na kidato cha sita 2024.