Mkaguzi wa Mifumo ya Ubora wa Mamlaka, Josephine Omodo (kulia), akielezea Miongozo ya Ukaguzi wa Ndani wa Mifumo ya Ubora ISO 9001:2015 na ISO 17025:2017 wakati wa kikao kazi Aprili 29, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyekaa katikati), Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora na `Usimamizi wa Vihatarishi, Benny Mallya (aliyekaa kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, Dkt. Shimo Peter (aliyekaa kushoto) wakiwa pamoja na Wakaguzi wa Ndani wa Mifumo ya Ubora kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) baada ya ufunguzi wa kikao kazi Aprili 29, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akizungumza wakati akifungua Kikao Kazi cha Wakaguzi wa Ndani wa Mifumo ya Ubora kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA),kinachofanyika katika ukumbi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Kibaha, Mkoa wa Pwani Aprili 29, 2024.
Mtumishi wa Mamlaka, Onesphat Stephano (kushoto) akitoa elimu juu ya majukumu ya Mamlaka kwa wananchi waliotembelea banda la Mamlaka katika maonesho ya Wiki ya Afya na Usalama kazini yanayofanyika katika viwanja vya General tyre jijini Arusha.
Mtumishi wa Mamlaka, Selina Maghembe (kulia) akitoa elimu juu ya majukumu ya Mamlaka kwa mtumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea banda la Mamlaka katika maonesho ya Wiki ya Afya na Usalama kazini yanayofanyika katika viwanja vya General tyre jijini Arusha Aprili 27, 2024.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA), Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka kwenye maonesho ya Wiki ya Afya na Usalama Kazini yanayofanyika katika viwanja vya General tyre jijini Arusha Aprili 27, 2024. Kulia ni Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Eliamini Mkenga.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Gerald Meliyo (kulia) wakimsikiliza Meneja Ubora wa Kiwanda cha kuchakata Pareto, Paul Looken (kushoto) akieleza namna wanavyofanya uchunguzi wa kimaabara kujua ubora wa mazao ya pareto wanayonunua kutoka kwa wakulima wakati wa ukaguzi wa maabara ya kiwanda hicho kilichopo Mafinga wilayani Mufindi uliofanyika kiwandani hapo Aprili 17, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia) na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Gerald Meliyo na Mkaguzi wa Kemikali, Revocatus Mwamba (kushoto) wakikagua stoo ya kemikali katika Kiwanda cha Lush Chanzo na kutoa maelekezo ya kufanyia kazi mapungufu waliyoyaona katika kiwanda hicho wakati wa ukaguzi uliofanyika Aprili 17, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto), akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Kiwanda cha Lush Chanzo, kufanyia kazi mapungufu yaliyoonekana upande wa chini wa matanki yanayotumika kuchanganya kemikali kwa ajili ya kutengeneza gundi inayotumika kutengenezea mbao za kutengeneza samani katika kiwanda hicho wakati wa ukaguzi uliofanyika Mafinga Aprili 17, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto), akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Kiwanda cha Lush Chanzo, kufanyia kazi mapungufu yaliyoonekana upande wa chini wa matanki yanayotumika kuchanganya kemikali kwa ajili ya kutengeneza gundi inayotumika kutengenezea mbao za kutengeneza samani katika kiwanda hicho wakati wa ukaguzi uliofanyika Mafinga Aprili 17, 2024.