Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Gerald Meliyo (kulia) wakitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Kiwanda cha Lush Chanzo, kufanyia kazi mapungufu yote waliyoyaona katika eneo la kuchanganya kemikali katika kiwanda hicho wakati wa ukaguzi uliofanyika Aprili 17, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kulia) akikagua nyaraka zilizobandikwa eneo la kuchanganyia kemikali zikieleza mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa kutumia kemikali katika kiwanda cha Lush Chanzo, wakati wa ukaguzi katika kiwanda hicho kilichopo eneo la Kinyanambo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Aprili 17, 2024. Kulia ni Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Gerald Meliyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala (wa tano kutoka kushoto) aliwa pamoja na timu ya washiriki pamoja na kamati ya maandalizi wa zoezi la utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi Tanzania (ZOKIKITA 2024) baada ya kuzinduliwa zoezi hilo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (mwenye tai nyekundu), akizungumza wakati akizindua zoezi la utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi Tanzania (ZOKIKITA 2024). Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji bandarini jijini Dar es Salaam Machi 14, 2024
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya uzinduzi wa zoezi la utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi Tanzania (ZOKIKITA 2024).
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala akitoa maelezo ya zoezi la utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi Tanzania (ZOKIKITA 2024) na mpango kazi wake kwa Waziri Mkuu (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka Profesa Esther Lugwisha (katikati) na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko (wa nne kutoka kushoto), wakiwa na watumishi kutoka Taasisi mbalimbali zinazofanyakazi katika mpaka wa Tanzania na Uganda (Mutukula), pamoja na watumishi wa Mamlaka baada ya kumaliza kikao na watumishi hao kilichofanyika katika mpaka wa Mutukula Machi 6,2024.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka Prof. Esther Lugwisha (wa pili kushoto), na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko (wa tatu kutoka kulia), wakimsikiliza Emmanuel Elias (kulia) msimamizi wa bwawa la kuhifadhia maji yenye kemikali yaliyotumika kuchenjua madini (Tailing Storage Facility) la mgodi wa GGM baada ya kutembelea bwawa hilo kwa ajili ya kuona namna wanavyosimamia kuhakikisha haliwezi kuleta madhara kwa wananchi endapo itatokea changamoto. Kushoto ni Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa, John Wanjala.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka Prof. Esther Lugwisha (katikati), akiwa na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto), wakitazama eneo linalohifadhi kemikali na bomba la dharula la kunawa baada ya mtu kupata madhara ya kemikali (Emergency Eye Wash).
Mwenyekiti wa Bodi na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko (waliosimama katikati), wakiwasikiliza wataalam wa kemikali wakieleza namna wanavyohifadhi na kutumia kemikali aina ya Cyanide kwenye shughuli za uchimbaji wa dhahabu katika mgodi wa GGM.