Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) Camillus Wambura (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, Dkt. Shimo Peter (wa pili kushoto), kuhusu huduma zinazotolewa na Mamlaka kwenye maonesho 49 ya Biashara ya Dar es Salaam wakati alipotembelea banda la Mamlaka kwenye Maonesho hayo, Julai 6,2025.
Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (kulia) akitoa elimu kuhusu majukumu mbalimbali ya Mamlaka kwa wananchi waliotembelea Banda la Mamlaka, kwenye maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam, Julai 6, 2025.
Mtumishi wa Mamlaka, Mussa Simon (kulia) akitoa elimu juu ya utunzaji wa Mazingira dhidi ya Kemikali taka kwa wananchi waliotembelea banda la Mamlaka kwenye maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 6, 2025.
Wananchi mbalimbali watembelea Banda la Mamlaka na kupata elimu juu ya majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 6, 2025.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, (kushoto), akitazama picha za matukio mbalimbali ya uchunguzi wa kisayansi wa dawa za kulevya wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. Kulia ni mtumishi wa Mamlaka Muhsin Kilonzo.
Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, Dkt. Shimo Peter (kulia), akitoa ufafanuzi kuhusu uchunguzi wa kimaabara unaofanywa na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mwananchi aliyetembelea banda la Mamlaka katika Maonesho Sabasaba
Watumishi wa Mamlaka (kulia) wakitoa elimu juu ya majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa wananchi waliotembelea banda la Mamlaka kwenye maonesho ya Sabasaba.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Sylvester Omary (kulia) akipokea maoni kutoka kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Mamlaka kwenye maonesho ya Sabasaba.
Mtumishi wa Mamlaka, Dereck Masako (kulia) akitoa maelezo kuhusu majukumu ya Mamlaka, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kushoto) alipotembelea banda la Mamlaka kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya yaliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma Juni 26, 2025.