CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

FAQ: 

What are GCLA services?

The following are the services provided by Government Chemist Laboratory Authority:-

 1. Laboratory Testing Analysis(Environmental,Industrial,Mineral,Food,Drugs,Microbiology,DNA,Forensic and Toxicology)
 2. Management and Control of Industrial and Consumer Chemicals
 3. Regulation of Human DNA services
 4. National Poison Control Centre(NPCC
 5. Implementation of three legislations, which are:
 •  The Government Chemist Laboratory Authority Act No.8 of 2016, which established GCLA as anAuthority
 •  The Industrial and Consumer Chemicals (Management and Control) Act No.3 of 2003, Cap 182
 • The Human DNA Regulation Act No. 8 of 2009, CAP 73.

Who is eligible to register to Customer Chemicals Management Portal (CCMP)?

All chemicals dealers within Tanzania Mainland are required to register to CCMP

What are the prerequisite requirement for Registration on the System?

During registration your required to attach two documents which are Tax Payer Identification Number (TIN) and Certificate of Incorporation from Tanzania Revenue Authority and Business Registration and Licensing Agency (BRELA) respectively.

How do I change a programme I have been admitted to?

During registration your required to attach two documents which are Tax Payer Identification Number (TIN) and Certificate of Incorporation from Tanzania Revenue Authority and Business Registration and Licensing Agency (BRELA) respectively.

Do I register If I was already registered manually?

Yes, All chemical dealers whether new or already registered manually will have to be registered with the Online Portal.

In re-registering with the Online Portal, do I need to remake payment?

No, All users that have already been registered will only attach receipts from the manual registration process.

If I have made payments with a mobile platform, where do I get the payment slip attachment?

For now, you can take a picture or a screenshot of the receipt message from your phone and upload it in place of the payment slip.

How many accounts can I have for 1 company?

You can only have 1 account per company.

Can I use my email as my username?

No, You can use any character or number but not any of the special characters (A minimum of 6 characters total). You can also use your name and some numbers.

What are the requirement's during application for Certificate?

During the application for Certificate the Company will have to choose the preferred Category, and each Category has different requirement's click here for more information.

Vinasaba ni nini ?

Vinasaba ni chembe ndogondogo za urithi ambazo hurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine na chembechembe hizi hubeba taarifa mbalimbali na muhimu za kibaiolojia zinazohusiana na kiumbe husika. Vinasaba hupatikana kwenye seli za mwili wa binadamu na viumbe wengine ikiwemo baadhi ya bakteria na virusi.Binadamu, hurithi nusu ya vinasaba (50%) kutoka kwa Mama na nusu nyingine(50%) ya vinasaba kutoka kwa Mama. Mpangilio wa chembechembe za vinasaba (DNA Profile) hutofautiana kwa mtu mmoja na mwingine isipokuwa kwa mapacha wenye kufanana(Identical twins).Mpangilio wa chembe chembe za vinasaba unaweza kubainisha uhalali wa watoto kwa wazazi pamoja na kubainisha mahusiano yaliyopo baina ya ndugu wa familia au ukoo mmoja

Taratibu za kupata huduma za uchunguzi wa vinasaba zikoje?

Huduma za uchunguzi wa vinasaba hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009.Taratibu zifuatazo hufuatwa ili kuweza kupata huduma za uchunguzi;-

 • Mteja anayehitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa vinasaba anawakilishwa na taasisi zilizotajwa kwenye sheria ili kumuombea mteja husika huduma za uchunguzi
 • Kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) cha Sheria ya vinasaba vya binadamu ya mwaka 2009, taasisi zinazoruhusiwa kumuombea mteja kupatiwa huduma za uchunguzi wa vinasabani pamoja na maafisa ustawi wa jamii, mawakili, mahakama, jeshi la polisi kwa masuala yanayohusu jinai n.k
 • Taasisi hizo zitaandika barua za maombi ya kupatiwa huduma za uchunguzi kwa niaba ya mteja husika. Barua zote zitaandika kwenda kwa mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali.
 • Malipo ya uchunguzi ni Tsh100, 000/=kwa sampuli ya mtu mmoja, hivyo kwa uchunguzi wa Baba,Mama na Mtoto jumla niTsh.300,000/=. Malipo yote hufanyika Benki
 • Baadaya ya kukamilisha taratibu za malipo, sampuli za mpanguso wa kinywa(Buccal swab ) zitachukuliwa na watalaam katika maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi kulingana na Maombi ya Mteja
 • Uchunguzi utafanyika na utakapokamilika majibu ya uchunguzi yatatolewa kwa taasisi iliyoandika barua ya maombi ya kufanyiwa uchunguzi na mteja husika atapata majibu yake kupitia taasisi hizo zilizoruhusiwa kisheria.
 • Majibu ya uchunguzi hutolewa kuanzia wiki ya pili baada ya kuchukuliwa kwa sampuli.

Matokeo ya uchunguzi wa vinasaba yakoje?

Matokeo ya uchunguzi wa uhalali wa watoto kwa wazazi ni ya uhakika.

 • Ikiwa baba anayepimwa si baba halalikibailojia, wa mtoto husika, uwezekano wa baba huyo kuwa ndiye baba mzaziwa mtoto husika ni asilimia sifuri (0%).
 • Ikiwa baba anayepimwa ni baba halalikibailojia, wa mtoto husika, uwezekano wa baba huyo kuwa ndiye baba mzaziwa mtoto husika ni asilimia 99.99 (99.99%).
 • Ikiwa Mama anayepimwa si Mama halalikibailojia, wa mtoto husika, uwezekano wa mama huyo kuwa ndiye mama mzaziwa mtoto husika ni asilimia sifuri (0%).
 • Ikiwa mama anayepimwa ni mama halalikibailojia, wa mtoto husika, uwezekano wa mama huyo kuwa ndiye mamamzaziwa mtoto husika ni asilimia 99.99 (99.99%).

Je Matumizi ya sampuli na taarifa za Vinasaba yanalindwa kisheria kisheria?

Teknolojia ya vinasaba vya Binadamu ni moja kati ya teknolojia zinazokuwa kwa kasi zaidi duniani,kwa kupitia matumizi ya vinasaba vya binadamu,teknolojia hii inaweza kutumika kuboresha ustawi wa maisha ya watu kwa namna mbalimbali.

Teknolojia hii ikitumika ipasavyo huweza kutumiwa katika uchunguzi wa magonjwa mbalimbali na tiba, pia huweza kutumika katika utambuzi wa binadamu,kubaini uhalali wa watoto kwa wazazi  na utambuzi viungo mbalimbali vya binadamu.

Vinasaba vya binadamu vimebeba taarifa nyingi na muhimu kuhusu binadamu, Kutokana na umuhimu huo Sheria ya vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009 ina lengo la  kudhibiti na kusimamia matumizi sahihi ya vinasaba vya binadamu.Sheria ya Vinasaba vya Binadamu imeweka utaratibu wa uchukuaji wa sampuli, kufungasha, usafirishaji , kuhifadhi,uchunguzi pamoja na kuteketezwa kwa sampuli baada ya kukamilika kwa uchunguzi

Mahitaji ya Kipimo cha Vinasaba Kabla ya kuchukuliwa kipimo cha vinasaba yakoje?

Mwombaji anapaswa apate barua ya maombi kutoka Mamlaka zinazotambulika kisheria ambazo ni:

 • Mahakama kwenye masuala ya jinai na kijamii
 • Mawakili waliosajiliwa na wanatambulika kisheria
 • Ustawi wa jamii
 • Polisi mwenye cheo cha kuanzia mkaguzi
 • Mkuu wa Wilaya kwenye majanga ya kitaifa.
 • Madaktari kwenye masuala ya matibabu
 • Taasisi au vituo vya utafiti vilivyosajiliwa

Gharama ya uchunguzi vinasaba zikoje?

Ghrama za uchunguzi ni  shilingi 100,000/= kwa sampuli moja yaani mtu mmoja. Hivyo kwa wahusika watatu (yaani baba, mama ma mtoto) ni shilingi laki tatu 300,000/=

Sampuli zipi huchukuliwa kwa ajii ya uchunguzi wa Vinasaba?

Sampuli itachukuliwa kutegemeana na mamlaka hitaji pamoja na taratibu za kitaaluma. Aina ya sampuli zinazochukuliwa mara nyingi ni mate au damu kwa sampuli linganishi. Sampuli za kutoka eneo la tukio itategemea na aina ya tukio.

Kituo cha kudhibiti matukio ya sumu nchini ni nini ?

Ni kituo cha kudhibiti matukio ya sumu nchini, kilichopo chini ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, kinachofanya kazi ya kudhibiti matukio ya sumu nchini kwa kushirikiana na taasisi za tiba ili kusaidia watu wanaoathirika na sumu.

Wadau wa NPCC ni nani?

Wadau wa NPCC ni mtu yeyote, anayeweza kukutana na tukio la sumu,aidha wadau wengine ni taasisi za tiba, hospitali, na wadau wengine wanaohusika katika kulinda afya za watanzania.

Nifanye nini ili kuweza kupata huduma hii ya tukio la sumu?

Ili kuweza kupata huduma za Kituo cha kudhibiti Sumu nchini  unatakiwa kupiga simu kwa namba za simu kwa namba 2113333 au 0736613333

Ni huduma gani naweza kupata kutoka kwenye kituo cha kudhibiti matukio ya sumu nchini?

Ushauri juu ya huduma ya kwanza kwa muathirika wa tukio la sumu, madhara ya sumu husika na ushauri wa kitaalamu kwa muathirika.

Tofauti kati ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA)

 • Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ina wajibu wa kulinda afya ya jamii kwa kuhakikisha ubora na usalama wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
 • Shirika la Viwango Tanzania (TBS) majukumu yake ni kusimamia na kulinda ubora wa bidhaa na chakula katika sekta ya viwanda na biashara
 • Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kisheria ndiyo Maabara Kuu ya Rufaa ya Serikali kwenye masuala yote yanayohusu uchunguzi wa kiamaabara na matokeo yake ni ya mwisho. Maabara pekee ya Serikali yenye jukumu la kufanya uchunguzi wa vielelezo vyote ikiwemo vielelezo vya vyakula na dawa pale vinapohusisha jinai au pale sampuli/vielelezo hivyo vinapohusisha maslahi ya taifa.

1. Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) inasajili nini?

 • Maabara za kemia zinazotumika viwandani na majumbani
 • Maabara za hospitali zinazofanya uchunguzi wa vinasaba vya binadamu
 • Waingizaji, watengenezaji, watumiaji, wasambazaji, watunzaji, wasafirishaji, wateketezaji na wasafirishaji wa kemikali nje ya nchi.
 • Kemikali kama zilivyoainishwa katika Majedwali namba 3, 6, 7 na 8 ya Sheria Na. 3 ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani ya mwaka 2003. Unaweza kuzitambua pia kemikali hizi kwa kutumia njia ya Harmonised Shipping Code (HS Code) zenye namba kuanzia 22.07 mpaka 40.05.

Shughuli zipi za kikemikali zinahitaji vibali kutoka GCLA?

Shughuli zinazohitaji vibali kutoka GCLA ni pamoja na kuingiza kemikali nchini, kusafirisha kemikali ndani ya nchi, kusafirisha kemikali nje ya nchi na kuteketeza kemikali taka

Ni wadau gani wa kemikali wanapaswa kusajiliwa na GCLA ?

 •  Nikitaka kusajili kemikali, maabara ya kemikali, mdau wa kemikali, maabara za sayansi jinai au maabara ya vinasaba vya binadamu nifanye nini?
 • Ukitaka kusajili kemikali, maabara ya kemikali au mdau wa kemikali utatakiwa kuingia kwenye mfumo wa e-Services unaopatikana katika tovuti ya GCLA. Katika Tovuti hiyo ingia  halafu ingia Customer Chemicals Management Portal, kisha ingia User Manual ambapo utapata maelekezo ya hatua kwa hatua ya jinsi ya kuanza usajili.
 • Ukitaka usajili wa Maabara ya sayansi jinai na Vinasaba vya Binadamu utatakiwa kutembelea Ofisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyopo karibu na wewe, ofisi hizo zipo katika kanda sita kama zinavyoonekana katika Our Contacts kwenye tovuti ya GCLA.

Ni huduma zipi za kiusimamizi wa kemikali zinahitaji malipo ili zikamilishwe na GCLA?

 • Usajili wa kemikali
 • Usajili maabara
 • Vibali vya kuingiza, kusafirisha na kuuza kemikali nje ya nchi
 • Ukaguzi wa kemikali
 • Uteketezaji wa kemikali taka
 • Usindikizaji wa kusafirisha kemikali hatarishi

Ni sampuli gani zinaweza kufanyiwa uchunguzi kwenye kurugenzi ya Uchunguzi wa Bidhaa na mazingira?

Ni sampuli za vyakula, dawa na malighafi za dawa, dawa asili, viungo vya chakula, vipodozi, maji taka, udongo, detergents, sediments,kemikali na mazao yake.

Ni nani wanaoweza kuleta sampuli kwa ajili ya uchunguzi?

Sampuli kwa ajili ya uchunguzi huweza kuletwa na wamiliki wa viwanda, wajasiriamali wakubwa na wadogo, mtu binafsi,Taaisisi za Serikali,mashirika binafsi na asasi zisizo za kiserikali.

Copyright ©2023 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.