Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea (kulia) akikabidhi cheti cha pongezi kwa mmoja ya wanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo ya sayansi wakati wa hafla ya kuwapongeza Wanafunzi na Walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati waliohitimu kidato cha nne mwaka 2023 na kidato cha sita 2024.
Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea, akitoa hotuba katika hafla ya kuwatunuku tuzo Wanafunzi na Walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne mwaka 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam Juni 12, 2025.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Christopher Kadio, akizungumza katika hafla ya kuwatunuku tuzo Wanafunzi na Walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne mwaka 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam Juni 12, 2025.
Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea (aliyevaa Kaunda suti) akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia) akieleza majukumu ya Mamlaka katika hafla ya kuwatunuku tuzo Wanafunzi na Walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati waliohitimu kidato cha nne mwaka 2023 na kidato cha sita 2024.
Wajumbe wa Menejimenti ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, wakifuatilia zoezi la utoaji tuzo kwa Wanafunzi na Walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati waliohitimu kidato cha nne mwaka 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam Juni 12, 2025.
Baadhi ya Wanafunzi waliofanya vizuri zaidi, wakiwa katika hafla ya kuwatunuku tuzo Wanafunzi na Walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati waliohitimu kidato cha nne mwaka 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam Juni 12, 2025.
Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shahibu Hassan Kaduara, akizungumza wakati akifungua maonesho ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya Madini wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Juni 11, 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mhe. Shahibu Hassan Kaduara (hayupo pichani) kufungua maonesho ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya Madini wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Juni 11, 2025.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi, Barnabas Essau (kulia), akipata elimu kutoka kwa Mtumishi wa Mamlaka, Chistina Englebeth (kushoto), kuhusu majukumu ya Mamlaka katika maonesho ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya Madini wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Juni 11, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akizungumza na wadau wa kemikali bashirifu zaidi ya 40 wakati akifungua kikao cha wadau hao na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kilichofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam, Mei 28, 2025.