Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

WANANCHI WAHIMIZWA USALAMA MAHALA PA KAZI

Imewekwa: 28 Apr, 2025
WANANCHI WAHIMIZWA USALAMA MAHALA PA KAZI

Mamlaka imewahimiza wananchi mbalimbali waliotembelea banda la Mamlaka katika Maonesho ya Kitaifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi kuzingatia usalama wanapokuwa kwenye maeneo yao ya kazi ili kuepuka madhara ya kiafya yanayoweza kuwapata.

Meneja wa Mamlaka ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Eliamini Mkenga ametoa rai hiyo Aprili 26, 2025 katika viwanja vya Mandewa mkoani singida kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi.

 "Kupitia uchunguzi wa kutambua aina ya dawa za kulevya, hili huleta usalama mahala pa kazi kwa kutambua watumiaji wa dawa za kulevya maeneo ya kazi kwani watumiaji wa dawa za kulevya wanaweza kusababisha ajali au akasababisha matatizo katika afya na mazingira. Hivyo, kwa kupata elimu itasaidia wadau kupima wafanyakazi wao ili kubaini kama wanatumia dawa za kulevya wakati wa kazi jambo ambalo litasaidia kuleta msimamo mahala pa kazi"
 

Pia, Meneja amewasihi wadau mbalimbali wanaojishughulisha na masuala ya kemikali kuhakikisha wanakamilisha taratibu zote zilizowekwa kwa ajili ya usalama mahala pa kazi ikiwemo kuwapa vifaa kinga wafanyakazi waliopo chini yao kwani afya ni mtaji katika maisha ya mwanadamu.

Kwa upande wake Saile kurata kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Mamlaka katika masuala ya uchunguzi wa vinasaba vya binadamu ili kujenga umoja katika jamii na pia kuwezesha watu kufanya kazi bila mawazo.

Maonesho ya Kitaifa ya Usalama na Afya mahala pa Kazi mwaka 2025 yamebebwa na kauli mbiu; Nafasi ya Akili Mnemba na Teknolojia za Kidijitali Katika Kuimarisha Usalama na Afya Mahala pa Kazi.