Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

WAKULIMA WAPEWA MBINU YA KUKABILIANA NA SUMU KUVU

Imewekwa: 11 Aug, 2026
WAKULIMA WAPEWA MBINU YA KUKABILIANA NA SUMU KUVU

Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo amewataka wananchi kuzitumia maabara za Mamlaka kuchunguza mazao ya kilimo ili kutambua usalama wake kabla ya matumizi.

Mkurugenzi Ndiyo amesema hayo Agosti 7, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa Habari waliotembelea Banda la Mamlaka katika maonesho ya Kitaifa Nanenane yaliyofanyika katika Viwanja vya Dkt. John Malecela, Dodoma.

“Unaweza kuwa na mazao yako kabla hujataka kuuza njoo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali tuchunguze kama ni salama kwa mlaji jambo linalomsaidia mkulima kuchukua hatua stahiki” alisema Ndiyo.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Ndiyo amewataka wakulima kuhakikisha wanazingatia mbinu za Kitaalamu wakati wa uvunaji ili kuepukana na Sumu kuvu.

“Katika wakati wa mavuno tuepukane na tabia ya kurundika mazao kwa makundi, lakini pia tuzingatia mbinu za kisasa za kuhifadhi ili kuepukana na tatizo la Sumu kuvu” alisema Ndiyo

Jackson Ibrahim na Mwiga Teka ni wakulima wanaoishi mkoani Singida, wameishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuwapa elimu ya kukabiliana na Sumu kuvu.

“Tunamshukuru Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kweli tumepata elimu nzuri na huwezi kuja kutoka Singida mpaka hapa Dodoma, Sumu kuvu inasumbua sana sasa tumejua namna ya kuikabili, Tunaomba Mkemia Mkuu wa Serikali afika mpaka huku chini atusaidie kutuelimisha zaidi kuhusu sumu kuvu na namna ya kuepuka” walisema.