MAMLAKA YANG’ARA TUZO ZA UBUNIFU KATIKA SEKTA YA UMMA 2025
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeibuka mshindi wa *Tuzo ya Ubunifu katika Sekta ya Umma, * ijulikanayo kama *"The Outstanding Regulatory Compliance and Safety in Chemical Management Award 2025"* ikiwa ni kutambua mchango mkubwa wa Mamlaka katika mabadiliko ya usimamizi na udhibiti wa kemikali na uboreshaji wa utoaji wa huduma kwa wananchi.
Tuzo hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Hamis Suleiman Hamis, ambaye alimuwakilisha Waziri wake, Mhe. Sharrif. A. Sharrif, katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam, ambapo tuzo hiyo ilipokelewa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, ambaye aliambatana na Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Evaclotida Kapinga, Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, Dkt. Shimo Peter na Katibu wa Mkemia Mkuu wa Serikali, Dorothy