Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

MAABARA YA MAIKROBAILOJIA YAPATA ITHIBATI

Imewekwa: 02 Apr, 2025
MAABARA YA MAIKROBAILOJIA YAPATA ITHIBATI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amesema Maabara ya Maikrobailojia ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kupata ithibati ya maabara ya kimataifa kutoka SADCAS.

Dkt. Mafumiko ameyasema hayo Machi 29,2025 wakati akifunga kikao cha kwanza cha Baraza la nane la wafanyakazi la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali lililofanyika katika ukumbi wa Dkt. Mafumiko, jijini Dodoma.

“Nina jambo moja la furaha nataka kuwaambia, ni kwamba Maabara yetu ya Maikrobaiolojia imepata ithibati ya kimataifa ya uchunguzi wa kimaabara kutoka SADCAS, haya ni mafanikio makubwa kwetu wote. Wakati nafika Mamlaka nilikuta maabara moja tu ya Chakula na Dawa ndiyo yenye ithibati na mpaka sasa maabara sita kati ya saba zimepata ithibati. Nataka mpaka kufikia wakati wa kumaliza muda wangu wa uongozi maabara zote ziwe na ithibati” alisema Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Mafumiko.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira, Dkt. Peter Shimo, amesema maabara hiyo imepata ithibati kutokana na juhudi kubwa za Taasisi nzima ili kuendana na mifumo ya ubora wa kimataifa jambo ambalo ni hatua kubwa kwa Mamlaka.

“Tumepata ithibati ya ISO 17025 ambayo inaiwezesha maabara na wataalamu kufanya uchunguzi na matokeo yake yanakubalika kitaifa na kimataifa na maana yake ni kuwa maabara inafuata mifumo yote ya ubora ya kimataifa” alisema Dkt. Shimo.