KIKAO CHA WAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt Fidelice Mafumiko amewataka watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuambukizana uzoefu ili kuongeza tija katika utendaji wa Taasisi huku akisisitiza kila mtumishi anajukumu la kuwajibika kwenye eneo lake ili kuongeza ufanisi wa Taasisi.
Mkemia Mkuu ameyasema hayo Juni 19, 2026 wakati akiongoza kikao cha Wafanyakazi wa Mamlaka kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
“Tuishi kwa kuambukizana ujuzi wale waliotangulia na wenye uzoefu mkubwa kwenye maeneo yote tuna jukumu la kuambukizana maarifa na ujuzi ili kujenga na kuiendeleza Taasisi yetu kuwa Imara, tunawapeleka Watumishi kwenye mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ili kuongeza Tija kwa taasisi ujuzi na maarifa yanayopatikana huko yazae manufaa kwa watumishi wote ni lazima urudi na ripoti” alisema Mkemia Mkuu wa Serikali
Jansen Bilaro na Martha Msola ni watumishi wa Mamlaka wenye uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Taasisi hii wao wanasema moyo wa Mamlaka umekuwa ni silaha hii ya kurithishana ujuzi kizazi hadi kizazi.
“Kila Taasisi ina misingi yake na desturi yake hapa kwetu kurithishana ujuzi na kubadilishana uzoefu ni silaha muhimu katika ustawi wa taasisi yetu kwa hiyo vijana wawatumie wakongwe na sisi tuwatumie vijana ili tusonge mbele” walisema watumishi hao.