Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

KAMISHNA GENERALI WA DAWA ZA KULEVYA AIPONGEZA MAMLAKA

Imewekwa: 30 Jan, 2024
KAMISHNA GENERALI WA DAWA ZA KULEVYA AIPONGEZA MAMLAKA

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa utoaji wa haraka wa ripoti za uchunguzi na uboreshaji wa mifumo ya utendaji kazi.

Kamishna Jenerali ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipotembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square.

“Nawapongeza kwa kuwahisha ripoti za uchunguzi na kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya sita kwa kununua mitambo imara na yenye ubora katika uchunguzi wa kimaabara na kupata ithibati za mifumo ya kimataifa” alisema Kamishna Jenerali.

Aidha, Kamishna Aretas Lyimo, alipongeza Mamlaka kwa kuwa na mifumo ya taarifa za uchunguzi wa kimaabara na wa taarifa za mashahidi wataalam ambayo inasaidia kubadilisha taarifa na wadau wengine wa haki jinai.

 “Nawapongeza pia kwa kuwa na mifumo ya kufanyia kazi ya kisasa, hii yote inasaidia kuongeza utendaji kazi na kusaidia vyombo vingine na Mahakama kwenye utendaji haki ili kuleta ustawi kwa Taifa” alisema.