Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

GCLA YATOA VIFAA VYA MAABARA VYENYE THAMANI YA ZAIDI MILIONI 4 KWA SHULE YA SEKONDARI GOGONI

Imewekwa: 19 Oct, 2023
GCLA YATOA VIFAA VYA MAABARA VYENYE THAMANI YA ZAIDI MILIONI 4 KWA  SHULE YA SEKONDARI GOGONI

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imetoa msaada wa vifaa vya maabara vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 4 kwa shule ya Sekondari ya Gogoni iliyopo Kibamba jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi vifaa hivyo Oktoba 14, 2023, katika Mahafali ya kumi na moja ya shule hiyo kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Meneja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa, amesema Mamlaka hiyo imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuwatia motisha wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi, kuweza kufanya vizuri kwenye masomo hayo.

Naomba niwakabidhi vifaa hivi kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, ikiwa ni mchango wake kwa shule hii ikiwemo kuhakikisha wanafunzi wanaosoma masomo ya Sanyansi wanapata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo kwa ufanisi.”alisema Mkapa.

Akipokea vifaa hivyo, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Charles Komba, ameishukuru Mamlaka hiyo kwa kuwapatia msaada huo, ambapo amesema vitawasaidia wanafunzi wanaochukua masomo ya Sayansi kuweza kufanya mafunzo kwa vitendo  vizuri tofauti na hapo awali walikuwa wakishindwa kufanya  kutokana na changamoto upungufu wa vifaa iliyokuwa ikiwabili.

Katika Hatua nyingine Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imetumia mahafali hayo kama jukwaa la kutoa elimu ya Matumizi salama ya kemikali ambapo wananchi waliohudhuria sherehe hiyo wameweza kupatiwa elimu hiyo ikiwemo elimu ya athari za kemikali endapo hazitotumiwa kwa uangalifu.