Kaimu Msimamizi wa Ofisi ndogo ya Dar es Salaam, Everlight Matinga (katikati) akifunga mafunzo ya Wasimamizi na Wachunguzi wa Maabara za Vinasaba vya Binadamu (hawapo pichani) mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Mkemia, jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 19 hadi 21, 2025.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya wasimamizi na wachunguzi wa Maabara za Vinasaba vya binadamu wakifuatilia mada kwenye mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mkemia, jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2025.
Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Baiolojia na Vinasaba, Dkt. Fidelis Bugoye (aliyesimama) akiwasilisha mada katika mafunzo ya Wasimamizi na Wachunguzi wa Maabara za Vinasaba vya Binadamu kwenye ukumbi wa Mkemia, jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2025.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na Takwimu, Omari Lugendo, akiwasilisha mada katika mafunzo ya Wasimamizi na Wachunguzi wa Maabara za Vinasaba vya Binadamu kwenye ukumbi wa Mkemia, jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2025
Mtumishi wa Mamlaka, Riphat Lusingo (kushoto) akizungumza wakati Wasimamizi na Wachunguzi wa Maabara za Vinasaba vya Binadamu walipotembelea maabara ya Vinasaba vya Binadamu katika Ofisi ndogo ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akiongea na viongozi wa Kampuni ya WASCO ISOAF Ltd wakati wa ukaguzi katika kampuni hiyo inayojihusisha na kuweka mpako joto (pipe coating) katika mabomba ya kusafirisha mafuta kwenye mradi wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda mpaka Chongoleani, Tanga iliyopo kijiji cha Sojo, Nzega, Tabora, Agosti 19, 2025. Katikati ni Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Magdalena Mkenga na kulia Mkaguzi wa kemikali, Revocatus Mwamba.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Magdalena Mtenga (wa pili kushoto), wakimsikiliza Meneja wa Maabara akieleza namna wanavyofanya uchunguzi wa sampuli mbalimbali za kuangalia ubora katika mradi huo wakati wa ukaguzi uliofanyika eneo la maradi Agosti 19, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kushoto), Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Magdalena Mtenga (kushoto), wakiwa pamoja na watumishi wa Mamlaka walioambatana nao wakimsikiliza Msimamizi wa Kemikali wa Kampuni ya WASCO, Kimbugwe Francis (wa tatu kushoto) akieleza namna kemikaliinavyotolewa kwenye matanki na kuingizwa kwenye eneo la kiwanda kwa ajili ya matumizi ya kuchanganya na kuweka mpako joto kwenye mabomba wakati wa ukaguzi uliofanyika Agosti 19, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati), Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Magdalena Mtenga (wa tano kulia), Mkurugenzi wa Kampuni ya WASCO ISOAF Ltd, Gary. Deason (wa tano kushoto) wakiwa pamoja na watumishi wa Mamlaka walioambatana nao na viongozi wa mradi huo mara baada ya kumaliza ukaguzi wa eneo la mradi huo uliopo kijiji cha Sojo, Wilaya ya Nzega, Tabora, Agosti 19, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Wakulima Nanenane, yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma, Agosti 8, 2025.