Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha utekelezaji na tathmini ya Watoa huduma za mitambo na vifaa vya Maabara kuendana na matakwa ya mifumo ya ubora kwa Wakurugenzi, Wataalam wa Mitambo ya Maabara, Wakuu wa Vitengo na Mameneja (Hawapo pichani), katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi NIMR, jijini Dar es Salaam, Oktoba 8, 2025.
Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora na Usimamizi wa Vihatarishi, Benny Mallya, akiwasilisha Taarifa ya Usimamizi wa Vifaa kwa Mtazamo wa Ubora katika kikao kazi cha utekelezaji na tathmini ya Watoa huduma za mitambo na vifaa vya Maabara kuendana na matakwa ya mifumo ya ubora kilichofanyika katika Ukumbi wa NIMR jijini Dar es Salaam, Oktoba 8, 2025.
Mtumishi wa Mamlaka, Adamu Mbugi, akiwasilisha Taarifa ya Mitambo ya Maabara katika kikao kazi cha utekelezaji na tathmini ya Watoa huduma za mitambo na vifaa vya Maabara kuendana na matakwa ya mifumo ya ubora kilichofanyika katika Ukumbi wa NIMR jijini Dar es Salaam, Oktoba 8, 2025.
Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi, Jerome Theogen, akielezea majukumu ya Idara Tumizi katika Mchakato wa Usimamizi wa Mikataba ili kuhakikisha Taasisi inafikia malengo ya Ubora kuanzia kwenye ununuzi hadi kwenye matumizi yake katika kikao kazi cha utekelezaji na tathmini ya Watoa huduma za mitambo na vifaa vya Maabara kuendana na matakwa ya mifumo ya ubora kilichofanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), jijini Dar es Salaam, Oktoba 8, 2025.
Baadhi ya Washiriki wa Kikao, wakifuatilia Mada mbalimbali katika kikao kazi cha utekelezaji na tathmini ya watoa huduma za mitambo na vifaa vya Maabara kuendana na matakwa ya mifumo ya ubora kilichofanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dar es Salaam, Oktoba 8, 2025.
Tuzo walizoshinda Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika mkoani Geita Septemba 27, 2025.
Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhe. Zena Ahmed Said (kulia), akikabidhi tuzo ya mshindi wa pili kwa Taasisi za Umma za Udhibiti kwa Meneja wa Sehemu ya Usajili na Ukaguzi wa Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu Fidelis Segumba (kati kati), na Boaz Mizar (kushoto), kwenye Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika mkoani Geita Septemba 27, 2025.
Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhe. Zena Ahmed Said (kulia), akikabidhi tuzo ya mshindi wa tatu kwa Taasisi Wezeshi za Serikali katika Sekta ya Madini kwa Meneja wa Sehemu ya Usajili na Ukaguzi wa Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu Fidelis Segumba, (kati kati), na Boaz Mizar (kushoto), kwenye Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika mkoani Geita Septemba 27, 2025.
Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhe. Zena Ahmed Said (kati kati), akiwa pamoja na washindi kutoka Taasisi mbalimbali walioshiriki Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika mkoani Geita Septemba 27, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama) akiongea katika kikao cha ufunguzi wa ukaguzi wa Mifumo wa Kiwango cha ISO 17025 kwa Maabara sita zilizopo Ofisi ndogo ya Dar es Salaam. Ufunguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mkemia, Dar es Salaam, September 23, 2025.