Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Dkt. Lazaro Mambosasa akizungumza wakati akifungua mafunzo ya usimamizi wa sampuli za sayansi jinai na usimamizi na udhibiti wa kemikali kwa maafisa wanafunzi wanaoendelea na kozi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam Machi 12, 2026.
Afisa kutoka Jeshi la Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam akiuliza swali wakati wa mafunzo ya uelewa juu ya masuala ya usimamizi wa sampuli za sayansi jinai na sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali yaliyofanyika Machi 12, 2026.
Maafisa Wanafunzi kutoka Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalam kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye mafunzo yaliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Kurasini Dar es Salaam, Machi 12, 2026.
Meneja wa Maabara Sayansi Jinai Baiolojia na Vinasaba, Dkt. Fidelis Bugoye akiwasilisha mada kuhusu usimamizi wa sampuli za sayansi jinai kwenye uchukuaji, uhifadhi, usafirishaji na utunzaji wa sampuli hizo kwa Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Polisi waliopo kozi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Mohamed Mdemu, kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali akiwakumbusha maafisa wanafunzi wa jeshi la Polisi (hawapo pichani), kuhusu umakini na weledi katika uchukuaji wa sampuli za jinai kwenye hatua za ufanyaji wa upelelezi wa kesi za jinai kwenye mafunzo yaliyofanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Dkt. Lazaro Mambosasa (aliyekaa katikati), akiwa pamoja na wataalam kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kufungua mafunzo ya uelewa juu ya usimalizi wa sampuli za sayansi jinai na sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali kwa Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam Machi 12, 2026.
Wanawake wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Makao Makuu na Kanda ya Kati - Dodoma, wakiwa tayari kuelekea katika Viwanja vya Mbande vilivyopo Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma yalipofanyika Maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2026, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.
Wanawake wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Makao Makuu na Kanda ya Kati - Dodoma, wakielekea katika Viwanja vya Mbande vilivyopo Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2026.
Wanawake wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Makao Makuu na Kanda ya Kati -Dodoma, wakiwa katika Viwanja vya Mbande vilivyopo Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma yalipofanyika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Machi 8, 2026, kwenye viwanja vya Barafu, Mburahati jijini Dar es Salaam.