Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamis Suleiman Hamis (wa tatu kulia) akimkabidhi Tuzo ya Ubunifu katika Sekta ya Umma, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati) ijulikanayo kama “The Outstanding Regulatory Compliance and Safety in Chemical Management Award 2025” iliyotolewa na Tanzania Public Service and Innovation Awards katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam, Desemba 16, 2025.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Christopher Kadio (kushoto) akizungumza wakati wa kikao kabla ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Kanda ya Mashariki kilichofanyika katika ukumbi wa Mamlaka, jijini Dar es Salaam, Desemba 18, 2025. Kulia ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko.
Mshauri Mwelekezi wa mradi wa ujenzi wa jengo la Kanda ya Mashariki kutoka kampuni ya CRJE, Rajabu Kihinga, akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo kwa viongozi (hawapo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mamlaka, jijini Dar es Salaam, Desemba 18, 2025.
Wajumbe wa Bodi wakifuatilia maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Kanda ya Mashariki jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mamlaka, jijini Dar es Salaam, Desemba 18, 2025.
Baadhi ya Viongozi wakifuatilia maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Kanda ya Mashariki jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mamlaka, jijini Dar es Salaam, Desemba 18, 2025.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Christopher Kadio (wa pili kutoka kulia) na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa maski) wakipata maelezo kutoka kwa Mshauri Mwelekezi wa mradi kutoka kampuni ya CRJE, Rajabu Kihinga (kushoto) walipo tembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka, Profesa Edda Vuhahula akitoa ushauri katika kuboresha maeneo mbalimbali kwenye ujenzi wa jengo la Mamlaka Ofisi ya Kanda ya Mashariki walipotembelea jengo hilo jijini Dar es Salaam, Desemba 18,2025.
Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Afya, Rahimu Masombo, akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Mwaka ya Uimarishwaji kwa wasimamizi wa kemikali kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mafunzo yanayofanyika kwa siku tatu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Kanda ya Mashariki kwenye ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha, Pwani Desemba 1, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akizungumza na wadau wa kemikali (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Afya, Rahimu Masombo (hayupo pichani) kufungua mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya yaliyofanyika Kibaha, Pwani, Desemba 1, 2025.
Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo, akiwasilisha mada kuhusu Muhtasari na Majadiliano ya majukumu ya Mamlaka katika Usimamizi na Udhiti wa Kemikali Kitaifa na Kimataifa katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo yaliyofanyika Desemba 1, 2025.