Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Afya, Rahimu Masombo, akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Mwaka ya Uimarishwaji kwa wasimamizi wa kemikali kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mafunzo yanayofanyika kwa siku tatu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Kanda ya Mashariki kwenye ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha, Pwani Desemba 1, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akizungumza na wadau wa kemikali (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Afya, Rahimu Masombo (hayupo pichani) kufungua mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya yaliyofanyika Kibaha, Pwani, Desemba 1, 2025.
Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo, akiwasilisha mada kuhusu Muhtasari na Majadiliano ya majukumu ya Mamlaka katika Usimamizi na Udhiti wa Kemikali Kitaifa na Kimataifa katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo yaliyofanyika Desemba 1, 2025.
Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa akiwasilisha mada kuhusu Muhtasari na Majadiliano ya majukumu ya Mamlaka katika Usimamizi na Udhiti wa Kemikali Kitaifa na Kimataifa katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo yaliyofanyika Desemba 1, 2025.
Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Afya, Rahimu Masombo (aliyekaa katikati) akiwa na viongozi kutoka Mamlaka pamoja na wadau wa kemikali baada ya kufungua Mafunzo ya Mwaka ya Uimarishwaji kwa wasimamizi wa kemikali yanayofanyika kwa siku tatu kwenye ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha, Pwani Desemba 1, 2025. Wa pili kutoka kushoto ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko.
Wadau wa kemikali wakiwasikiliza wawezeshaji kwenye Mafunzo ya Mwaka ya Uimarishwaji kwa wasimamizi wa kemikali yanayofanyika kwa siku tatu kwenye ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha, Pwani, Desemba 1, 2025.
Mtumishi wa Mamlaka kutoka Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Michael Bernard, akiwasilisha mada kuhusu usimamizi wa usalama wa kemikali (Chemical Safety Management) kwenye Mafunzo ya Mwaka ya Uimarishwaji kwa wasimamizi wa kemikali yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha, Pwani, Desemba 1, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akiongea wakati akizindua Kamati ya Pili ya Utafiti ya Mamlaka uliofanyika katika ukumbi wa Mkemia, jijini Dar es Salaam, Novemba 11, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia) akimkabidhi Sera na miongozo ya kusimamia Utafiti, Mwenyekiti wa Kamati ya Pili ya Utafiti ya Mamlaka, Dkt. Fidelis Bugoye (kushoto)
Wajumbe wa Kamati ya Utafiti ya Mamlaka, wakimsikiliza Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Utafiti ya Mamlaka