Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akiongea wakati akizindua Kamati ya Pili ya Utafiti ya Mamlaka uliofanyika katika ukumbi wa Mkemia, jijini Dar es Salaam, Novemba 11, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia) akimkabidhi Sera na miongozo ya kusimamia Utafiti, Mwenyekiti wa Kamati ya Pili ya Utafiti ya Mamlaka, Dkt. Fidelis Bugoye (kushoto)
Wajumbe wa Kamati ya Utafiti ya Mamlaka, wakimsikiliza Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Utafiti ya Mamlaka
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (Katikati waliokaa) akiwa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Pili ya Utafiti ya Mamlaka mara baada kuizindua Novemba 11, 2025, Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (hawapo pichani), wakati akifungua mafunzo kwa Wakaguzi wapya wa Kemikali na Maabara za Kemia yaliyofanyika katika Ofisi za Kanda ya Mashariki zilizopo kwenye jengo la Ushirika, Dar es Salaam, Novemba 10, 2025.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyekaa katikati), akiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo (wa pili kushoto, waliokaa), Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa (wa pili kulia), wawezeshaji pamoja na wakaguzi wapya wa Kemikali na Maabara za Kemia baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa wakaguzi hao yaliyofanyika katika Ofisi za Kanda ya Mashariki katika jengo la Ushirika jijini Dar es Salaam Novemba 10, 2025.
Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo, akiwasilisha mada kuhusu Mikataba ya Kimataifa inayohusiana na Udhibiti na Usimamizi wa Kemikali.
Watumishi wa Mamlaka wakifuatilia mada mbalimbali katika Mafunzo kwa Wakaguzi wapya wa Kemikali na Maabara za Kemia.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao cha pili cha Baraza la Nane la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Cate Hotels mkoani Morogoro Oktoba 24, 2025.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamalaka, wakifuatilia ajenda zilizokuwa zinawasilishwa katika siku ya pili ya kikao cha pili cha Baraza la Nane la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.