Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Kanzidata ya Maktaba kwa watumishi wa Makao Makuu na Ofisi ya Kanda ya Kati (hawapo pichani), yaliyofanyika katika ukumbi wa Dkt. Mafumiko Dodoma, Aprili 2, 2026.
Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora na Usimamizi wa Vihatarishi, Benny Mallya, akiongea kabla ya kumkaribisha Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, (hayupo pichani) kufungua mafunzo ya Kanzidata ya Maktaba kwa watumishi wa Makao Makuu na Ofisi ya Kanda ya Kati yaliyofanyika katika ukumbi wa Dkt. Mafumiko Dodoma, Aprili 2, 2026.
Baaadhi ya watumishi wa Mamlaka, Makao Makuu na Ofisi ya Kanda ya Kati, wakifuatilia wasilisho katika mafunzo ya Kanzidata ya Maktaba yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Dkt. Mafumiko Dodoma, Aprili 2, 2026.
Msimamizi wa Maktaba, Nuriati Hamisi akiwasilisha mada juu ya jinsi ya kutumia Kanzidata mbalimbali za maktaba kwa Watumishi wa Mamlaka Makao Makuu na Ofisi ya Kanda ya Kati (hawapo pichani) kwenye mafunzo ya Kanzidata ya Maktaba yaliyofanyika katika ukumbi wa Dkt. Mafumiko Dodoma, Aprili 2, 2026.
Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo, akizungumza na wadau wa Maabara za Kemia (hawapo pichani) wakati akifungua Mafunzo ya Udhibiti na Usimamizi wa Maabara za Kemia yaliyofanyika katika Hoteli ya Zabibu, jijini Dodoma, Machi 31,2026.
Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Magdalena Mtenga, akiwasilisha mada kuhusu Majukumu ya Mamlaka kwa Wadau wa Maabara za Kemia (hawapo pichani) katika Mafunzo ya Udhibiti na Usimamizi wa Maabara za Kemia yaliyofanyika katika Hoteli ya Zabibu, Dodoma Machi 31,2026.
Mtumishi wa Mamlaka, Fidelis Chrizant akiwasilisha mada kwa wadau wa maabara ya kemia (hawapo pichani) kuhusu Umuhimu wa usajili wa kemikali na maabara za kemia walioshiriki mafunzo ya Udhibiti na Usimamizi wa Maabara za Kemia yaliyofanyika Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo (aliyekaa katikati), Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Magdalena Mtenga (wa pili kushoto, waliokaa) wakiwa pamoja na watumishi wa Mamlaka, Kanda ya Kati pamoja na Wadau wa Kemikali na Maabara za Kemia waliohudhuria Mafunzo ya Udhibiti na usimamizi Kemikali na Maabara za Kemia yaliyofanyika katika Hoteli ya Zabibu, jijini Dodoma, Machi 31,2026.
Waziri wa Afya, Mhe. Mohammed Mchengerwa, akizungumza wakati akifungua Mkutano na Wataalam wa Tiba Asili uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji Mtumba, Dodoma, Machi 25, 2026.
Waziri wa Afya, Mhe. Mohammed Mchengerwa (kulia), akimsikiliza Kaimu Meneja wa Maabara ya Maikrobaiolojia, Alois Ngonyani, (kushoto), akitoa maelezo namna Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inavyofanya kazi katika uchunguzi wa Dawa za Tiba Asili katika Mkutano wa Mhe. Waziri wa Afya na Wataalam wa Tiba Asili uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji Mtumba, Dodoma, Machi 25, 2026.