Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Gerald Meliyo (kulia) wakimsikiliza Meneja Ubora wa Kiwanda cha kuchakata Pareto, Paul Looken (kushoto) akieleza namna wanavyofanya uchunguzi wa kimaabara kujua ubora wa mazao ya pareto wanayonunua kutoka kwa wakulima wakati wa ukaguzi wa maabara ya kiwanda hicho kilichopo Mafinga wilayani Mufindi uliofanyika kiwandani hapo Aprili 17, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia) na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Gerald Meliyo na Mkaguzi wa Kemikali, Revocatus Mwamba (kushoto) wakikagua stoo ya kemikali katika Kiwanda cha Lush Chanzo na kutoa maelekezo ya kufanyia kazi mapungufu waliyoyaona katika kiwanda hicho wakati wa ukaguzi uliofanyika Aprili 17, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto), akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Kiwanda cha Lush Chanzo, kufanyia kazi mapungufu yaliyoonekana upande wa chini wa matanki yanayotumika kuchanganya kemikali kwa ajili ya kutengeneza gundi inayotumika kutengenezea mbao za kutengeneza samani katika kiwanda hicho wakati wa ukaguzi uliofanyika Mafinga Aprili 17, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto), akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Kiwanda cha Lush Chanzo, kufanyia kazi mapungufu yaliyoonekana upande wa chini wa matanki yanayotumika kuchanganya kemikali kwa ajili ya kutengeneza gundi inayotumika kutengenezea mbao za kutengeneza samani katika kiwanda hicho wakati wa ukaguzi uliofanyika Mafinga Aprili 17, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Gerald Meliyo (kulia) wakitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Kiwanda cha Lush Chanzo, kufanyia kazi mapungufu yote waliyoyaona katika eneo la kuchanganya kemikali katika kiwanda hicho wakati wa ukaguzi uliofanyika Aprili 17, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kulia) akikagua nyaraka zilizobandikwa eneo la kuchanganyia kemikali zikieleza mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa kutumia kemikali katika kiwanda cha Lush Chanzo, wakati wa ukaguzi katika kiwanda hicho kilichopo eneo la Kinyanambo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Aprili 17, 2024. Kulia ni Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Gerald Meliyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala (wa tano kutoka kushoto) aliwa pamoja na timu ya washiriki pamoja na kamati ya maandalizi wa zoezi la utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi Tanzania (ZOKIKITA 2024) baada ya kuzinduliwa zoezi hilo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (mwenye tai nyekundu), akizungumza wakati akizindua zoezi la utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi Tanzania (ZOKIKITA 2024). Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji bandarini jijini Dar es Salaam Machi 14, 2024
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya uzinduzi wa zoezi la utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi Tanzania (ZOKIKITA 2024).
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala akitoa maelezo ya zoezi la utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi Tanzania (ZOKIKITA 2024) na mpango kazi wake kwa Waziri Mkuu (hayupo pichani).